PSG wamtolea uvivu Neymar
Rais wa klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa Nasser Al-Khelaifi ameamua kuweka wazi msimamo wa klabu hiyo na kinachoendelea kuhusiana na nyota wao wa Kibrazil Neymar.
Kwa siku za hivi karibuni zimezuka tetesi kuwa Neymar amekuwa hana furaha katika klabu ya Paris Saint Germain na wengine wakieleza kuwa nyota huyo anajutia uamuzi wake wa kuihama FC Barcelona 2017 kwa dau la euro milioni 222 na kuweka rekodi ya dunia na kujiunga na PSG.
Khelaif amenukuliwa na France Football akikanusha kuhusiana na mchezaji huyo kutokuwa na furaha Paris huku akisisitiza kuwa hakuna mtu aliyewahi kumlazimisha Neymar kusaini kuichezea PSG.
.
“Ninataka mchezaji anayeweza kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya jezi (PSG) , kwa wale ambao hawataki kufanya hivyo au kuelewa hilo tutaonana kila mmoja na kuongea nao.
Hakuna aliyemlazimisha Neymar kusaini kwetu.Hakuna aliyemsukuma. Anajua alikuja kujiunga na hii Project.” alisema CEO huyo wa PSG Nasser Al-Khelaifi