Moja kati ya tukio la heshima tutakaloliona ni kiungo wa England U-21 anayeichezea pia Leicester City ya Ligi Kuu nchini England James Maddison kutoa heshima kwa rafiki yake wa karibu marehemu Sophia wakati wa michezo ya mataifa ya Ulaya kwa chini ya miaka 21 ambayo imeanza juzi Juni 16.
.
James Maddison Januari alimpoteza rafiki yake Sophia,5, kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani ya mifupa na kupelekea kifo chake, kwa heshima ya Sophia Tylor aliyefariki mwaka mmoja baada ya kugundulika kuwa ana kansa ya mifupa akiwa na umri wa miaka mitano kiungo huyo ametengenezewa kiatu maalum chenye picha ya marehemu Sophia atakivaa katika michezo ya England U-21 kwenye michuano hiyo ya Ulaya ikiwa kama njia ya kumuenzi.
Binti huyo alikuwa shabiki wa Norwich City alikutana na James Maddison Aprili 2018 lakini baada ya kuhamia Leicester James alimualika tena Sophie atembelea King Power na kushuhudia mechi mwezi Desemba.
Mwezi Machi mwaka huu akiwa anaichezea Leicester City, alipofunga goli la free-kick dhidi ya Burnley, alivua jezi na kuonesha maandishi katika nguo ya ndani yakisema “ RIP Sophie I Love You” , picha hiyo akishangilia goli hilo, imejumuishwa katika kiatu chake hicho maalumu atakachovaa katika michuano ya Ulaya.