Kocha wa Paraguay aponda timu kualikwa Copa America
Baada ya sare ya 2-2 ya Paraguay na Qatar jana katika mchezo wa kundi B kwenye michuano ya Copa America 2019, kocha wa timu ya Taifa ya Paraguay Eduardo Berizzo ameliponda shirikisho la soka la Amerika kusini CONMEBOL kwa kuzialika timu za nje ya bara hilo kwenye michuano hiyo.
Mabingwa wa Asian Cup 2019 Qatar pamoja na washindi wa pili kombe hilo Japan wamealikwa kushiriki michuano hiyo ya Copa America mwaka huu ambayo inashirikisha timu 12.
Hii ni mara ya kwanza Qatar kushiriki michuano hiyo na kuwa nchi ya kwanza ya kiarabu kucheza Copa America, huku Japan ikiwa ni mara yao ya pili kualikwa katika Copa America, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999.
.
“ Sijawahi kuona Ulaya wakialika timu yoyote kutoka America kusini.
Ninafikiri itakuwa na maana kubwa kucheza Copa America na timu zote kutoka America..” alisema kocha huyo wa Paraguay Eduardo Berizzo kufuatia ya timu yake kupata sare baada ya magoli yote mawili waliyokuwa wakiongoza kurudishwa na wapinzani wao Qatar.