Kagere ajitia kitanzi Simba
Mshambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere ambae ni raia wa nchini Rwanda ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Klabu yake ya Simba SC.
Katika msimu mmoja aliojiunga na Simba SC Kagere amekuwa mfungaji bora aliefikisha magoli mengi katika msimu wa 2018/2019 kwa kuwa na magoli 23.
Pia katika tuzo za Mo Simba Awards za msimu huu amekuwa Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa mwaka katika tuzo hizo.