Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewapa klabu ya Yanga uwanja huko Kigamboni, ambapo klabu hiyo kupitia mwenyekiti wake Mshindo Msolla wamesema watautumia uwanja huo kujenga kituo (Academy) ya kukuza vipaji.
Makonda ametoa ahadi hiyo katika hafla ya uchangishaji ya timu hiyo iliyofanyika leo Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.