Carragher amkazia Van Dijk mbele ya Messi
Sasa moja kati ya tuzo zinazokuwa zinasubiriwa kwa hamu katika soka ni pamoja na tuzo ya Ballon d’Or 2019, kwa miaka 10 iliyopita kabla ya mwaka jana kuchukua Luka Modric ilikuwa tuzo hiyo inatawaliwa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao walikuwa wakipokezana.
Kwa mwaka 2019 hadi sasa inatajwa kuwa Cristiano Ronaldo hapewi nafasi kutwaa tuzo hiyo lakini Lionel Messi wa Barcelona na Virgil van Dijk wa Liverpool ndio kama wanashindanishwa kwa karibu na mmoja kati yao anadaiwa kuwa ndio anaweza kutangazwa.
Licha ya wengi kimpigia chapuo sana Virgil kushinda tuzo hiyo, nyota wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka Jamie Carragher ametaja kuwa haoni namna ya mchezaji huyo kushinda.
“Namuona (Virgil) akienda kushindana na Lionel Messi katika tuzo hiyo, kwa kubashiri naona Messi akienda kushinda tena tuzo hiyo, ni nadra sana kwa beki wa kati kushinda Ballon d’Or, ninafikiri Fabio Canavaro alishinda kwa sababu ya mgongo wa kutwaa Kombe la Dunia 2006, lakini kiukweli (Virgil) amekuwa na msimu mzuri” alisema Carragher