Ronaldo ageuka wakala, ataka kumleta De Ligt Juventus
Baada ya mechi ya fainali kati ya Ureno na Uholanzi kumalizika hapo jana, Cristiano Ronaldo alimfuata beki wa Uholanzi na nahodha wa Ajax Matthijs de Ligt na kumwambia ajiunge na Juventus.
.
“Ronaldo aliniuliza kuhusu kuja Juventus. Nilishangazwa na kidogo na lile swali,ndio maana nilicheka. Mara ya kwanza sikumuelewa….Kwa hiyo sikusema chochote.” Alisema De Ligt akihojiwa na chombo cha habari cha Uholanzi,NOS.
De Ligt,19, ambaye anawindwa na klabu kubwa barani Ulaya kama vile Man United,Liverpool,PSG pamoja na Juventus, anatazamiwa kuondoka Ajax katika majira haya ya kiangazi.
Beki huyo wa kati amesema kuwa kwa sasa anaenda kwenye mapumziko na atafikiria ni kipi bora kwake halafu atafanya maamuzi.