Nadal abeba ubingwa French Open 2019
Rafa Nadal anaendelea kuwa Mfalme wa Clay Court.
Katika mchezo wa fainali ya French Open 2019 jana dhidi ya Dominic Thiem wa Austria, Nadal ameibuka na ushindi wa seti 6-3,5-7,6-1,6-1.
Hii ni mara ya 12 Mhispania huyo anachukua ubingwa wa michuano hii ya French Open, na pia ni mara ya tatu mfululizo anachukua ubingwa huo.
Nadal,33, sasa amechukua jumla ya Grand Slams 18 katika maisha yake ya Tenesi.