Msifikirie Jose Mourinho hapendi kushambulia anapenda ila…
Jumamosi Manchester United ilicheza mchezo wa 11 wa Ligi Kuu Uingereza ugenini na wenyeji wao AFC Bournemouth na mchezo ulimalizika kwa Manchester United kupata mataokeo ya ushindi wa magoli 2-1 yaliowapa alama tatu muhimu katika Ligi Kuu.
Mshambuliaji Marcus Rashford ndio ameiokoa Manchester United na sare ya 1-1, baada ya kufunga goli la ushindi dakika za majeruhi na kuipa ushindi Manchester United, baada ya mchezo huo kocha wa Manchester United Jose Mourinho alikiri mbele ya waandishi kuwa hawakuwa vizuri bali walikuwa na bahati, inawezekana ni kutokana na Bournemouth kupata goli la mapema zaidi dakika ya 11 kuptia kwa Callum Wilson ambaye alisaidia timu yao kujiamini zaidi.
“Baada ya mapumziko kwenda tukiwa 1-1 niliamini kuwa mImi ndio kocha mwenye bahati zaidi Ligi Kuu, Kiukweli tulikuwa na bahati sana kwa sababu tulikuwa wabovu, sehemu ya ulinzi imesaidia kiukweli, naupenda ule wimbo shambulia, shambulia, shambulia lakini unatakiwa kujua wakati unapopoteza mpira una uwezo wa kuzuia?” alisema Jose Mourinho
Walau ushindi huo uliopatikana kwa magoli ya Anthony Martial dakika ya 35 na Rashford dakika za lala salama, unaisogeza Manchester United hadi nafasi ya 7 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza wakiwa na jumla ya alama 20 wakati AFC Bournemouth wakilingana alama na Manchester United baada ya leo kulingana alama wote 20 wakicheza michezo 11 kila timu.