Mfalme wa Clay Court atinga fainali ya 12
Mfalme wa Clay Court Mhispania Rafa Nadal ameshinda mechi ya nusu fainali ya michuano French Open 2019 kwa seti 6-3, 6-4, 6-2 dhidi ya Mswiss Roger Federer.
Nadal ambaye ni bingwa mara 11 wa michuano hiyo, hii ni mara ya 12 anafuzu hatua ya fainali ya French Open.
Mhispania huyo ambaye ni bingwa mara mbili mfululizo wa michuano hiyo, atacheza fainali na mshindi kati ya Novak Djokovic na Dominic Thiem.