Messi akiri kum-miss Ronaldo
Mara kadhaa imewahi kuripotiwa kuwa uongozi wa juu wa LaLiga haukuzipokea kwa furaha taarifa za nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kuhama Real Madrid na kujiunga na Juventus ya Italia, LaLiga inadaiwa waliona kuwa Ligi yao imeondokewa na mchezaji muhimu ambaye ana mashabiki wengi.
Kwa LaLiga hiyo ilikuwa shida kwao , nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi aliwahi kunukuliwa kuwa Real Madrid wamepoteza mchezaji muhimu na watamkumbuka sana lakini inaelezwa kuwa hawakulipokea kwa uzuri na kubisha baadhi ya watu mtandaoni ikiwemo kumpinga Messi.
Messi akizungumza na Fox Sports hivi karibuni ameeleza kuwa sio tu LaLiga ndio inamkumbuka Ronaldo hata yeye anamkumbuka,kwani uwepo wake ulikuwa unaleta ushindani baina yao na kila mmoja alikuwa akitamani kuwa bora zaidi kila mwaka.
“Nilisema hilo wakati msimu unaanza na baadhi ya watu Madrid wakaanza kupata hasira na kauli yangu lakini ni ukweli, hivi unawezaje kutomkumbuka mchezaji ambaye msimu mmoja anafunga magoli zaidi ya 50? Kilichotokea Madrid (Bila ya Ronaldo) kingeweza kutokea katika timu yoyote ambayo Ronaldo angekuwa anaichezea halafu akahama” alisema Lionel Messi