Koeman ampigia Debe Van Dijk kushinda Ballon d’Or mbele ya Messi
Michuano ya klabu Bingwa Ulaya imemalizika huku tukishuhudia timu zenye majina ya wachezaji nyota kama FC Barcelona wakiwa na Lionel Messi na Juventus wakiwa na Cristiano Ronaldo kuondolewa katika michuano hiyo na kushindwa kufika fainali.
Wengi wameanza kuhoji ni nani anastahili kupewa tuzo ya Ballon d’Or 2019 ikiwa Lionel Messi na Ronaldo hawajafanya vizuri sana wakiwa na timu zao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa? Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi ambaye amewahi kuifundisha Everton ya nchini England Ronald Koeman amempigia chapuo beki wa Liverpool Mholanzi Virgil van Dijk kuwa ndio anastahili.
.
“( Van Dijk) anastahili kushinda Ballon d’Or “ alisema Koeman jana jumatatu.
Mara nyingi hupewa wachezaji wanaofunga au kutengeneza magoli ya uamuzi, lakini kama kuna wakati wa kumpa beki tuzo hiyo huu ndio wakati wake”
.
“Messi ni mchezaji mzuri, lakini ili kutwaa tuzo hiyo ninafikiria pia ni lazima ushinde mataji makubwa na timu yako ili kuwa mshindani” alisema Koeman