Shabiki wa Valencia aliyepoteza uwezo wa kuona aenziwa kiaina yake
Klabu ya Valencia ya nchini Hispania imeamua kutambua mchango wa shabiki wao aliyekuwa mlemavu wa macho ikiwa ni miaka miwili imepita toka kitokee kifo chake.
Valencia wameamua kumuenzi kwa heshima shabiki huyo kwa kumtengenezea sanamu katika siti yake aliyokuwa akipenda kukaa katika uwanja wa Mestalla.
Shabiki huyo wa Valencia anayejulikana kwa jina la Vincente Aparicio alipata ulemavu wa macho miaka 40 iliyopita akiwa na umri wa miaka 54 baada ya retina ya macho yake kupata matatizo.
Pamoja na kupoteza uwezo wa kuona hiyo haikumfanya kuachana na mchezo wa soka na badala yake aliendelea kuwa shabiki mkubwa wa Valencia kwa miaka 40 huku akiwa anakata tiketi za msimu mzima.