Makonda amwaga Mamilioni Simba
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametimiza ahadi yake ya kuwazadia washindi wa tuzo za msimu wa Klabu ya Simba.
Washindi wa tuzo hizo wamepewa kila mmoja milioni moja huku kipa Aishi Manula akipewa Tsh Milioni 10 na mkuu wa mkoa huyo ambapo amesema kuwa hela hiyo amemzawadia kwa kazi kubwa aliyofanya nchini Congo katika mechi ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.
Mechi hiyo ya marudiano iliisha kwa Simba kupoteza kwa goli 4-1 na Simba kutolewa kwenye michuano.