Anthony Joshua apigwa kwa mara ya kwanza
Mmexico Andy Ruiz Jr ameshinda pambano lake dhidi ya Muingereza Anthony Joshua kwa TKO katika Raundi ya saba leo Madison Square Marekani.
Hii ni mara ya kwanza AJ anapoteza pambano.
Katika pambano hilo Ruiz Jr amemuangusha AJ chini mara nne.
Bondia huyo ambaye alikuw hapewi kipaumbele kushinda pambano hilo, ameishangaza dunia na kwa ushindi huo na hivyo kufanikiwa kuondoka na mikanda yote mitatu ya IBF,WBO na WBA iliyokuwa inamilikiwa na Joshua.