Reyes wa Arsenal afariki Dunia
Nyota wa zamani wa Sevilla na Arsenal Mhispania Jose Antonio Reyes amefariki dunia leo Juni Mosi kwa ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 35.
Ajali hiyo imetokea leo huko nchini Hispania.
Timu ya mwisho kuichezea kabla ya kufariki ilikuwa ni Extremadura UD ya Hispania inayoshiriki Segunda Division au LaLiga2.
Reyes alijiunga na Arsenal mwaka 2004 akitokea Sevilla, na msimu wake wake Arsenal alishinda ubingwa wa ligi kuu ambapo walimaliza msimu wakiwa hawajapoteza mchezo.