Kenyatta amwaga mamilioni kwa wanamichezo Kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa pesa za Kenya zaidi ya milioni 181 ( Tsh Bilion 4) kwa wanamichezo wa Kenya kama malipo ambayo walistahili kupewa kutokana na ushiriki wao katika mashindano tofauti tofauti kama Olympic na Jumuiya ya madola.
Kenyatta pamoja na kuhakikisha pesa hizo wanapewa lakini amemuagiza waziri wa michezo wa Kenya ndani ya miezi mitatu aje na sera ya fidia kwa wanamichezo lakini wanamichezo wa Kenya wanapokuwa wanaondoka kwenda nje ya nchi kuhakikisha wanahudumiwa na mfuko wa taifa wa michezo.
Pesa hizo amezitoa jana katika Ikulu ya Kenya ikiwa ni kukamilisha malipo ya mabingwa hao wa michezo mbalimbali wa tangu mwaka 2010.
Wanamichezo hao 3,338 walioshiriki katika matukio 32 ya kimichezo wamelipwa pesa hizo pamoja na kupewa token ya Ksh milioni 2 (Tsh Millioni 45) kama pongezi.