Grealish atoa siri ya viatu vyake
Baada ya miaka mitatu klabu ya Aston Villa imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya nchini England kwa msimu wa 2019/2020 kufuatia ushindi wa 2-1 wa mchezo wa Championship Playoff dhidi ya Derby County hapo jana katika uwanja wa Wembley.
Gumzo la mchezo huo lilikuwa ni nahodha wa Aston Villa, Jack Grealish ambaye alikuwa anaamini katika bahati zaidi .
Jack Grealish katika mchezo huo alivaa kiatu kibovu ambacho kilishika macho ya watu wengi, wakishangaa mchezaji huyo anayelipwa pauni 25,000 kwa wiki (Tsh milioni 72.9) kuvaa kiatu kama kile.
Baada ya mchezo huo uliowapandisha ligi kuu,Jack Grealish akiongea na Sky Sports alielezea stori yake na kiatu hicho kilichochokaa.
Grealish alisema alivyotoka majeruhi mwezi Machi mwaka huu, alianza kuvaa viatu hivyo ambapo vilikuwa ni vipya kabisa, wakati anavivaa akaweza kufunga magoli kadhaa na kupata assists.
Hivyo akawaza kuwa hivyo ni viatu vyake vya bahati, ikabidi avihifadhi na jana akavivaa na kweli wakafanikiwa kushinda na kurejea katika ligi kuu nchini England.