Steve Kerr azua gumzo baada ya kukutana Popovic
Kocha wa Warriors Steve Kerr siku chache nyuma ameonekana akiwa Dinner na kocha wa San Antonio Spurs Gregg Popovich huko San Francisco,California.
Hii imeleta maswali kwa watu wengi wakisema kuwa huenda Popovich anampa mbinu Steve Kerr jinsi ya kumzuia Kawhi Leonard katika fainali za NBA.
Popovich alikuwa kocha wa Kawhi akiwa Spurs kabla ya mchezaji huyo kutimkia Toronto Raptors mwaka jana.
Mechi ya kwanza ya fainali hizo itachezwa Ijumaa hii Mei 31 katika uwanja wa Raptors,Scotiabank Arena.