Wanasoka waliopata bahati ya kucheza na Ronaldo na Messi timu mmoja
Pamoja ya kuwa Dunia ya soka hadi leo inaamini kuwa hakuna mchezaji/wachezaji bora waliowahi kufikia uwezo wa Diego Marado wa Argentina na Abeid Pele wa Brazil lakini huwezi kuacha kuwapa heshima Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Ronaldo amekuwa mshindani mkubwa wa Messi lakini mara kadhaa amewahi kuongea mbele ya waandishi wa habari kuwa wao (Ronaldo na Messi) ndio wachezaji bora kutokana na wamewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kwa miaka zaidi ya saba kitu ambacho hakijawahi kutokea katika kizazi hiki.
Hivyo kutokana na umahiri wa wachezaji hao baadhi ya wachezaji au watu wa familia ya soka wanaamini ukicheza timu mmohja kati ya Ronaldo na Messi badi utakuwa ni mchezaji mwenye bahati, hii ndio orodha ya wachezaji waliowahi kupata bahati ya kucheza na Ronaldo na Lionel Messi kati ka timu mmoja.
1- Carlos Tevez ni moja kati ya wachezaji waliopata bahati ya kucheza na Ronaldo na Messi katika timu moja, Tevez amacheza na Ronaldo kwa miaka miwili walipokuwa wote katika klabu ya Manchester United kuanzia 2007-2009 na amcheza na Messi pia timu ya taifa ya Argentina kutokana na wao kuwa wanatokea taifa moja.
2- Angel Di Maria huyu ni moja kati ya wachezaji hao yeye alipata bahati ya kucheza na Cristiano Ronaldo kwa miaka minne kuanzia 2010 hadi 2014 wakiwa Real Madrid lakini amecheza na Lionel Messi upande wa timu ya taifa ya Argentina.
3- Gonzalo Higuan nae amepata bahati ya kucheza Ronaldo katika klabu ya Real Madrid nchini Hispania kwa miaka minne kuanzia 2009-2013, huku Lionel Messi akiwa mchezaji mwenzake timu ya taifa ya Argentina.
4- Kwa upande wa mreno Deco de Souza alipata bahati ya kucheza na Lionel Messi kwa miaka minne tu kuanzia 2004-2008 ndani ya klabu ya FC Barcelona lakini alikuwa akicheza timu ya taifa ya Ureno na Cristiano Ronaldo kwa muda mrefu..
5- Gerard Pique aliwahi kucheza Manchester United kuanzia 2004-2008na hiyo ndio ilikuwa fursa nzuri kwake ya kucheza na Cristiano Ronaldo katika timu hiyo kabla ya miaka minne baadae kuamua kurudi kwao Hispania na kujiunga na FC Barcelona anayoichezea hadi leo hii wakiwa na Lionel Messi.