Kidiaba apewa shavu na Rais wa Congo
Ni siku nne zimepita tokea Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi kumtangaza waziri mkuu katika serikali yake baada ya kumtoa Joseph Kabila katika kiti cha Urais alichokalia kwa miaka 18.
Sasa Rais Felix ameanza kuunda serikali yake na kuweka watu anaoamini wanaweza kumsaidia.
Kocha wa makipa wa TP Mazembe na mlinda mlango wa zamani wa timu hiyo Robert Kidiaba ameonekana kuwa katika orodha ya watu wanaoaminiwa sana na Rais Tshisekedi kufikia hatua ya kupewa uwaziri wa michezo wa taifa la congo.
Kidiaba (43) aliyecheza TP Mazembe kwa miaka 16 na kuamua kustaafu kazi hiyo 2016 na kuanza kuwa kocha wa makipa wa TP Mazembe, ameendeleza maisha yake mazuri katika kazi yake ya siasa, hiyo ikiwa ni miezi michache imepita toka ashinde Ubunge wa Jimbo la Katanga jijini Lubumbashi Congo DR.