Timu ya Samatta yapata pigo
Kiu ya miaka nane ya klabu ya KRC Genk kutotwaa taji la Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji ilimalizika kwa msimu huu wa 2018/2019 kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuibwaga Club Brugge ambao walikuwa wakiwapa changamoto kwa muda mrefu.
KRC Genk wataingia msimu ujao kwa kuanza kutetea taji hilo pasipo uwepo wa kocha wao mkuu Philippe Clement (47) aliyekuwa akiifundisha timu hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, Clement baada ya Ubingwa huo licha ya kubembelezwa na uongozi wa juu wa KRC Genk ametangaza kwenda kutafuta changamoto mpya.
Kocha Clement sasa rasmi ameamua kuhamia kambi ya upinzani Club Brugge na ndio ataifundisha msimu ujao.
Clement awali amewahi kuitumikia Club Brugge katika nafasi za kocha wa muda, msaidizi na skauti wa timu hiyo, hivyo kwa maana hiyo safari yake na KRC Genk kama kocha aliyoianza Desemba 18 2017 imehishia hapa.