FIFA Yachemka kuongeza timu kombe la Dunia 2022
Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA linaonekana kuchemka na mpango wake kabambe wa kutaka michuano ya Kombe la Dunia kuanzia 2022 inayotarajiwa kuchezwa nchini Qatar kuwa na jumla ya timu 48.
Maamuzi ya kuongeza timu kufikia 48 yalishakubaliwa kuanza katika kombe la Dunia mwaka 2026 likalofanyika nchi za USA,Mexico na CANADA, lakini mwaka jana Rais wa FIFA Gianni Infantino alisema ongezeko hilo la timu linaweza kuanza mwaka 2022.
Mabadiliko hayo yangeilazimu Qatar kuchangia uenyeji wa michuano na nchi nyingine
Shirikisho la soka hilo limesema kuwa, baada ya mashauriano ya kina sasa mabadiliko hayo hayataweza kufanyika mwaka 2022.
Maamuzi hayo yanatarajiwa kutangazwa rasmi Juni 5 katika mkutano mkuu wa FIFA utakaopangwa kufanyika Paris nchini Ufaransa.