Wachezaji saba wa Yanga kuwakosa Mbeya City
Kikosi cha Yanga SC kesho kitashuka Dimbani dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru huku kikiwakosa wachezaji wake saba ambao wote ni wagonjwa.
Akizungumza na Wolrdsport14 Mratibu wa Klabu ya Yanga Hafidhi Salehe amesema kuwa wachezaji hao watakao kosekana ni Beki Vicent Andrew “Dante” anaumwa homa , Beki Said Juma ‘Makapu’ homa , Mshambuliaji Ibrahim Ajib anaumwa Dengue, Beki Paul Godfrey ‘Boxer’ homa , Winga Mrisho Ngasa homa
Beki Juma Abdul homa pamoja na Kiungo Mohamed Issa ‘Banka’ homa
Hafidhi ameongeza kuwa kwa sababu Mabeki wengi hawatakuwa sehemu ya mchezo huo itabidi wawatumie wachezaji wa Yanga B ili kuzima mapengo yaliyopo na wanaamini watafanya vizuri katika mchezo huo.