Ajax watoa ubingwa wao kwa mchezaji wao aliyeacha soka baada ya kuumia Ubongo
Baada ya miaka miwili toka kiungo wa Ajax Abdelhak Nouri (22)alazimike kustaafu mchezo wa soka baada ya kupata majeraha kwenye ubongo, klabu ya Ajax imeuelekeza ubingwa wao wa Ligi Kuu nchini Uholanzi kwa Abdelhak kama heshima kwa kijana huyo ambaye amesitisha maisha ya soka.
.
Ajax ambao timu yao imejaa damu changa imefikia maamuzi hayo kwa kuutoa Ubingwa huo kwa nyota huyo kama sehemu ya kuonesha mapenzi na jitihada zake kwa klabu hiyo licha ya lengo lake la kucheza soka la ushindani kwa muda mrefu kufutika akiwa bado mdogo.
Ubingwa huo waliochukua Ajax wa 34 wa Ligi Kuu Uholanzi kuwahi kuchukua lakini pia unaendana na namba ya jezi aliyokuwa anavaa Abdelhak Nouri kabla ya kulazimika kustaafu ili kuokoa maisha yake.
Nouri amepewa heshima hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ajax kutwaa taji hilo baada ya miaka mitano kupita.
.
Abdelhak aliumia ubongo 2017 katika mchezo wa kirafiki kati ya Ajax dhidi ya Wender Bremen baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.