Mwenyekiti wa Yanga ashangazwa na usajili wa Makambo
Baada ya taarifa kusambaa juu ya Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Heritier Makambo kusaini mkataba wa miaka mitatu na timu ya Hoyora AC ya nchini Guinea,Klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake Mshindo Msolla amesema kuwa wanamsubiri Kocha mkuu wa Klabu hiyo Mwinyi Zahera aje atoe ufafanuzi juu ya suala hilo.
.
Msolla amesema kuwa Kocha Zahera na mchezaji wake Makambo waliaga kuwa wanaenda nchini Guinea kucheki Afya na mambo yanayoendelea mitandaoni nao wanashangaa maana sio makubaliano yao na Kocha huyo.
.
“Mwalimu Zahera na Makambo maombi yao yalikuwa akapime Afya kwa hiyo hayo tuliyoyaona akisaini na kuvaa jezi ngoja warudi ili Mwalimu atatufafanulia vizuri,
Maana haiwezekani mchezaji akawa na mkataba wa mwaka mmoja alafu asaini timu nyingine bila kufuata taratibu za Klabu” Msolla
.
Msolla ameongeza kuwa Heritier Makambo bado ni mali ya Yanga na bado anamkataba wa mwaka mmoja na anaofa tatu za Klabu zinazomtaka.
.
“Makambo bado ni mali ya Yanga na mpaka sasa ana ofa tatu hivyo tutaangalia nani anaofa kubwa ndio tutamuuza mchezaji wetu” Msolla