Ndanda watamba kuifunga Simba
Klabu ya Ndanda FC kupitia kwa Katibu wake mkuu Selemani Kachele amesema kuwa watahakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Simba SC.
Kachele amesema kuwa pamoja na Simba SC kuwa na timu nzuri lakini wana madhaifu ambayo mwalimu wao anayafanyia kazi ili waweze kuyatumia madhaifu hayo na kuweza kuwafunga maana Simba wanafungika.
“Nikweli Simba SC ni timu nzuri lakini pia wana madhaifu yao ambayo mwalimu wetu ameyafanyia kazi madhaifu yao ili tuweze kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi yao na sio kwamba Simba hawafungiki pamoja na ubora wao lakini wanafungika” Kachele
Simba SC atakuwa mwenyeji wa Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa Mei 19 mwaka huu saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.