Berahino afungiwa miezi 30
Baada ya kuthibitika na kubaini kuwa nyota wa Burundi na timu ya Stoke City ya nchini England Saido Berahino ametenda kosa la kuendesha gari akiwa amelewa, Mahakama nchini England imetangaza adhabu yake baada ya kupitia shauri lake kwa miezi mitatu.
Saido (25) amebainika kuwa mwezi Februari 18 aliendesha gari lake aina ya Range Rover jijini London akiwa amelewa kitu ambacho ni kinyume na taratibu za sheria ya udereva wa magari duniani kote.
Kutokana na kutenda makosa hayo Berahino amepewa adhabu ya kufungiwa kwa miezi 30 kuendesha gari pamoja na faini ya pauni 75000.
Berahino anakuwa nyota wa pili wa soka katika kipindi kifupi kukutwa na hatia ya makosa ya barabarani na Mahakama, baada ya David Beckham nae kufungiwa miezi sita gari kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa anatumia simu