Meneja wa Taifa Stars aeleza sababu ya kambi kuchelewa
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kuanza Kambi juni 1 mwaka kabla ya kuelekea nchini Misri kwaajili ya kucheza fainali ya Kombe la mataifa Afrika AFCON ambapo Misri ndio mwenyeji wa fainali hizo.
Fainali hizo zinatarajiwa kuanza juni 21 mpaka julai 19 mwaka huu nchini humo
Meneja wa Taifa Stars Danny Msangi amesema kuwa sababu za kuchelewa kuweka Kambi ya timu ya taifa ni kutokana na wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa bado wapo wanazitumikia timu zao, ambapo baada ya Ligi kuu Tanzania bara kumalizika Mei 28 mwaka huu,ndipo wataingia Kambini kwenye timu ya taifa.
.
“Sababu ya timu kuchelewa kuingia kambini ni kutokana na wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa bado wapo kuzitumikia timu zao ambapo Ligi kuu Tanzania bara ikiisha mwezi huu tarehe 28, Kocha Amunike ametoa siku kadhaa za wachezaji hao kupumzika na ndipo waingie kambini” Msangi
Taifa Stars atakuwa na mchezo wa kirafiki nchini Misri dhidi ya Faraho,utakaochezwa Juni 13 mwaka huu.
Pia Msangi ameongeza kuwa mchezo mmoja wa kirafiki hautatosha hivyo watafanya jitihana za kuweza kupata mchezo mwingine wa kirafiki na timu ambayo itakuwepo nchini Misri.
.
” Mchezo mmoja hautoshi kujipima kwa timu yetu hivyo tunatarajia kuwa na michezo ya kirafiki miwili ili kuweza kujipima vizuri tutakapokuwa nchini Misri kabla ya michuano kuanza” Msangi