Ajib asema wamerudisha matumaini ya Ubingwa
Baada ya Ushindi wa jana wa goli 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ,Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema wamefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Ajibu amesema kabla ya ushindi huo baadhi yao walishaanza kukata tamaa kutokana na kupoteza michezo miwili mfululizo.
Amesema baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa na kupoteza mchezo uliopita wa ligi kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Biashara United, wengi walijua wataendelea kupoteza tena.
.
“Matokeo mabaya huwa yanatutoa kwenye mstari kabisa, tunamshukuru Mungu haya matokeo yatatufanya tujiamini upya na kuendelea kukaa kwenye mbio za ubingwa,”Ajibu
.
Ajibu ameongeza kuwa Kocha wao Mwinyi Zahera, anajua timu yake imecheza vipi na wapi afanye marekebisho, anaamini kabla ya kumalizia michezo miwili iliyobaki watakuwa wamefanyia kazi makosa yote ambayo yamejitokeza.
.
Ajibu amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani katika michezo iliosalia ili kuwapa hamasa wachezaji na kufanya vizuri.
.
Yanga imebakisha mechi mbili ambazo ni dhidi ya Mbeya City mchezo utakaochezwa Mei 22 na Azam FC utakaochezwa mwisho wa msimu Mei 28.