Shujaa wa United kuchezesha fainali Klabu Bingwa Ulaya
Shirikisho soka Ulaya UEFA ikiwa siku zinahesabika kuelekea mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya limemtangaza mwamuzi wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur za nchini England mchezo ambao utachezwa katika jiji la Madrid Hispania.
.
UEFA kimemtangaza muamuzi Damir Skomina (42) raia wa nchini Slovenia ndio atachezesha mchezo huo wa fainali unaozikutanisha timu za taifa moja, Skomina hii ndio itakuwa fainali yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwahi kuchezesha ila amekuwa na uzoefu wa michezo ya Ulaya kwa muda mrefu.
.
Tukukumbushe, Damir Skomina ndiye mwamuzi aliyechezesha mchezo wa 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya PSG dhidi ya Manchester United jijini Paris, mchezo ambao ulimalizika kwa penati tata iliyoamuliwa na VAR na kuwapa ushindi Manchester United na kuitoa PSG dakika ya 94.