Griezmann awaaga Atletico Madrid
Baada ya kudumu ndani ya klabu ya Atletico Madrid kwa miaka mitano akitokea Real Solcadad ya nchini Hispainia, Mfaransa Antoine Griezmann ametangaza rasmi kuondoka katika kikosi hicho hukua akiwa hajaweka wazi anaelekea timu gani.
Griezmann ambaye amekuwa na wakati mzuri ndani ya klabu hiyo ametajwa kuwa anaondoka na kwenda kujiunga na Mabingwa wa LaLiga klabu ya FC Barcelona ambao wanaendelea kuimarisha timu yao.
Hadi anatangaza kuongoka Griezmann aliye na umri wa miaka 28 inadaiwa akitua Nou Camp atapewa kandarasi ya miaka mitano, wakati huu akiwa anaondoka Atletico Madrid baada ya kucheza kwa miaka mitano akiwa kafunga jumla ya mabao 133 katika michezo 256 na kutoa pasi 50 za usaidizi wa magoli huku akiwa kashinda mataji matatu makubwa Europa League, Supercopa de Espana na UEFA Super Cup.