PSG wavunja rekodi ya miaka 58
PSG imevunja rekodi ya miaka 58 ya klabu ya Tottenham Hotspur barani Ulaya baada ya ushindi wao dhidi ya Lille jana na kuwafanya wawe wameshinda mechi 12 mfululizo katika mwanzo wa msimu wa league 1.
Rekodi iliyopita ya kushinda mechi nyingi mfululizo mwanzoni mwa msimu katika ligi tano kubwa barani Ulaya ilikuwa inashikiliwa na Tottenham Hotspur ambao walishinda mechi 11 msimu wa 1960-61.
Katika mechi hiyo ambayo PSG walikuwa nyumbani kwao Parc des Princes, Kylian Mbappe ndiye aliyefunga goli la kwanza kunako dakika ya 70, likiwa ni goli lake la 13 kwenye mechi 11 alizocheza msimu huu.
Mbrazil Neymar Jr akafunga goli la pili katika dakika ya 84, na goli la kufutia machozi la Lille likafungwa Nicolas Pepe dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati.
Mabingwa hao wa France sasa wapo kileleni mwa ligi kwa pointi 11 juu ya Lille ambao wapo nafasi ya pili.