Raioa afungiwa baada ya kuita shirikisho la soka dhaifu
Mambo yanazidi kumuendea mlama wakala wa mchezaji wa Manchester United Paul Pogba Mino Raiola, wakala huyo ambaye ni mzaliwa wa Italia siku chache zilizopita shirikisho la soka nchini Italia (FIGC) lilitangaza kumfungia miezi mitatu kutokufanya shughuli zozote za uwakala katika nchi hiyo kwa miezi mitatu.
.
Baada ya adhabu hiyo kutokana ni kama FIGC imemwagia moto mafuta na shirikisho la mpira wa miguu la dunia kuamua kuirefusha adhabu hiyo na kuwa kidunia sio tu nchini Italia, hivyo Raiola kwa sasa hawezi kufanya kazi za uwakala kwa mchezaji yoyote katika nchi yoyote hadi Agosti 9 2019 na hivyo usajili wa Pogba kwenda Real Madrid uliotajwa kufanyika majira ya kiangazi unaweza usifanyike baada ya doa hilo kuingia.
.
Adhabu hiyo inakuwa ni pigo kubwa kwa Mino Raiola ambaye ndio kipindi chake hiki cha kupiga hela kufuatia dirisha la usajili barani Ulaya ndio linaelekea kufunguliwa huku Raiola akitajwa kuwa ni wakala wa wachezaji mbalimbali zaidi 20.
Sababu kuu zilizosababisha FIGC na FIFA wamfungie hazijatajwa hadharani ila inatajwa kuwa kauli yake ya kuliita shirikisho hilo la Italia ‘dhaifu’ na haliendelei ndio imepelekea hayo yote, japo wengine wanasema kuwa ana shutuma nyingine nyuma ya pazia.
.
Dirisha la usajili nchini England linafunguliwa Mei 16 na kufungwa Agosti 8, siku moja kabla ya adhabu ya Mino Raiola kumalizika wakati nchini Italia dirisha la usajili litakuwa linafungwa Agosti 19, baadhi ya wateja wa Mino Raiola ni pamoja na Mario Balotteli, Mkhitaryan, Moise Kean na Lorenzo Insigne.