PSG hawajakubaliana na kifungo cha Neymar
Uongozi wa Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa ikiwa zimepita saa kadhaa toka shirikisho la mpira wa miguu nchini ufaransa (FFF) kutangaza kumfungia mechi tatu nyota wa timu hiyo Neymar, wametangaza kuwa watakata rufaa kwani hawaoni sababu za msingi kwa nyota wao huyo raia wa Brazil kuadhibiwa kwa madai ya kumsukuma shabiki aliyedawai kumkera Neymar na kumtusi.
Mwezi uliopita Neymar akiwa na PSG walipoteza kwa penati 6-5 dhidi ya Rennes katika mchezo wa fainali ya Copa de France uliyomalizika 2-2, hivyo wakati wanapanda kuchukua medali za mshindi wa pili Neymar alionekana mwenye jazba na kumsukuma shabiki anayedaiwa kuwa aliwatukana wachezaji wa PSG akiwemo Neymar.