Jurgen Klopp awajia juu UEFA
Kuelekea mchezo wa fainali ya Europa League ambao umepangwa kuchezwa Mei 29 nchini Azerbjain katika mji wa Baku kwa kuzikutanisha timu za Chelsea na Arsenal, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ambao wao watacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa na Tottenham katika mji wa Madrid amewasikitikia mashabiki wa Chelsea na Arsenal wataokwenda kuangalia fainali hiyo Baku.
Kocha huyo raia wa Ujerumani amewashangaa waliopanga fainali hiyo mjini Baku kutokana na umbali wa kwenda huko na uwezekano wa usafiri kutokuwa wa uhakika.
.
“Kwenda Baku kwa mchezo wa fainali ya michuano ya Ulaya inachekesha kidogo, hawa watu waliofanya maamuzi ya kupeleka fainali ya Europa League Baku sijui walipata nini wakati wa kifungua kinywa, unawezaje kufanya hivyo, sijui hata kidokezo chochote cha kufika kule au kama kuna ratiba ya kawaida ya ndege kufika huko” alisema Jurgen Klopp.
.
Jurgen Klopp amewataka watu wanaofanya maamuzi haya wawe wanatumia busara zaidi na maamuzi yao yawe ya kuridhisha.
.
Kutoka mjini London zinapotokea Arsenal na Chelsea hadi Baku ni Kilomita 3967 ambao ni umbali mrefu.