Hakuna refa atakayekataa VAR
Kukiwa bado na vuta ni kuvute kwa baadhi ya nchi kuamua rasmi kuingiza matumizi ya mfumo wa kiteknolojia katika maamuzi tata katika mchezo wa soka Video Assistant Referee, kwa upande wa baadhi ya waamuzi wameonesha kuunga mkono suala hilo.
Kwa watu wa kawaida wamekuwa wakiona VAR kama inaondoa utamu wa mchezo halisi lakini kwa mujibu wa refa wa Scotland Willie Collum amesema hakuna mwamuzi duniani atakayechukizwa na uwepo wa teknolojia ya VAR.
Willie Collum ameyaeleza hayo wakati wa mahojiano maalum na BBC kuhusina na faida watakazo zipata Scotland kwa kutumia teknolojia ya VAR katika mchezo wa soka huku akisema VAR itafaidisha soka la Scotland “Hakuna muamuzi yoyote katika hii dunia ambaye hatounga mkono VAR na itakuwa ni rahisi kwa wachezaji kukubali maamuzi”