Chelsea na Arsenal wafanyiwa ukatili fainali Europa League
Baada ya michezo ya Europa League kumalizika usiku wa Mei 9 2019 na kujua kuwa sasa fainali Mei 29 itakuwa inazikutanisha timu za England za Chelsea na Arsenal zikiwa zinatokea jiji moja la London, utaratibu wa mashabiki wao kupata tiketi umetangazwa rasmi.
.
UEFA wametangaza kuwa kuelekea mchezo huo wa fainali utakaochezwa nchi Azerbaijan katika mji wa Baku kwenye uwanja wa Olympic, mashabiki wa timu za Chelsea na Arsenal kila moja watapewa tiketi 6000 katika uwanja unaochukua mashabiki 68700.
.
Huku tiketi nyingine zilizosalia zitauzwa kwa mfumo wa kawaida kuwawezesha wanaopenda kuangalia mchezo huo.
.
Gharama ya tiketi za klabu itakuwa kuanzia pauni 26 hadi 121 (Tsh elfu 77 hadi laki 3) huku tiketi za mashabiki wengine (Majority) zitakuwa zikiuzwa kwa pauni 43 (Laki moja na elfu 20)
.
Arsenal wamesema kuwa wamesikitishwa ugawaji huo wa tiketi.
“Kutakuwa na maelfu ya mashabiki ambao wamekuwa wakiiunga mkono timu kwa miaka na wamekuwa sehemu ya safari yetu ya Europa Ligi msimu huu,ambao watakosa kuhudhuria.” Wamesema Arsenal.
.
Liverpool na Tottenham wao kila mmoja amepewa tiketi 16,613 kwa ajili ya mchezo wao wa fainali utakaochezwa Juni 1, kwenye uwanja wa Atletico Madrid Wanda Metropolitano unaochukua mashabiki 68,000.