Hazard kutegua kitendawili baada ya fainali ya Europa
Nyota wa kikosi cha Chelsea ambaye kwa muda mrefu amekuwa midomoni mwa watu na vyombo vya habari kuwa msimu huu ukimalizika anaweza kutimka wakati wowote, huku klabu ya Real Madrid ikitajwa kuwa ndio chaguo lake, ameendelea kuacha maswali na kushindwa kuweka wazi msimamo wake.
Hazard baada ya kuiwezesha timu yake ya Chelsea kwa kuifungia penati ya 4-3 ya ushindi katika mchezo wa nusu fainali ya Europa League dhidi ya Frankfurt baada ya dakika kumalizika 1-1 huku wakilingana kila kitu, amegoma kueleza msimamo wake kama anaondoka au la zaidi ya kusema ana hakikisha anaipambania Chelsea ishinde Europa League.
.
“Sifikiri kuhusiana na hilo, nafikiria kuhusiana na kushinda taji kwa ajili ya hii na hichi kikosi basi.
Kama ni mechi yangu ya mwisho nitajitahidi kufanya kila kitu kama sivyo tutataona. Katika kichwa changu sijui bado, ninafikiria tu kushinda mechi.” Alizungumza Hazard baada ya kuulizwa kama fainali ya Europa League ndio itakuwa mechi ya mwisho kwake kuichezea Chelsea.