Beki aliyekuwa anawindwa na Simba ajitia kitanzi Azam
Beki wa kimataifa kutoka nchini Ghana anayecheza Klabu ya Azam Yakubu Mohamed ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Klabu hiyo.
Msemaji wa Klabu hiyo Jaffary Idd Maganga amesema kuwa baada ya Uongozi wa Klabu hiyo tayari umeishazungumza na mchezaji huyo na kufikia hatua ya kuongeza mkataba wa miaka miwili.
.
“Yakubu leo hii alikuwa na mazungumzo na viongozi wa Klabu yetu na mazungumzo yamekamilika na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kuitumikia Azam FC” Maganga
Jaffary pia amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa Azam FC kuwa zile taarifa za kuwa Beki huyo anaenda katika Klabu ya Simba SC,taarifa hizo si za ukweli na Yakubu bado ni mali ya Azam FC.
.
“Kulikuwa na taarifa kuwa Yakubu tayari ameishamaliza taratibu za kujiunga na Klabu ya Simba , nipende kuwaambia wapenzi na mashabiki wa Klabu yetu kuwa Yakubu bado yupo Azam FC na leo ameongeza mkataba wa miaka miwili na leo atakuwa sehemu ya wachezaji katika mechi yetu dhidi ya KMC itakayochezwa saa 2.00 usiku” amesema Maganga