Rufaa ya Chelsea yakataliwa FIFA
FIFA wameikataa rufaa ya Chelsea waliyoikata dhidi ya kifungo cha kufanya usajili kwa madirisha mawili walichopata mwezi Februari mwaka huu.
Chelsea walipata kifungo hicho baada ya kuvunja sheria za usajili kwa wachezaji wa kigeni walio chini ya miaka 18.
Chelsea wameeleza kuwa baada ya rufaa yako kukataliwa sasa wataenda katika mahakama ya michezo ya kimataifa (CAS)