Kocha wa Simba ashinda tuzo ya mwezi tena
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi April katika ligi kuu Tanzania Bara akiwashinda kocha wa Azam FC Abdul Mingange, na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera waliokuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho.
Hii ni mara ya pili kwa Kocha huyo kuweza kuchaguliwa kuwa Kocha bora wa mwezi tangu alipojiunga na Klabu ya simba Julai 19 mwaka 2018.Na ni mara pili mfululizo anachukua tuzo hiyo.