Vardy ashinda tuzo ya mwezi England
Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April ligi kuu nchini England.
Katika mwezi huo Vardy amefunga magoli matano katika mechi nne alizocheza.
Vardy ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda Eden Hazard, Jordan Henderson, Aymeric Laporte, Shane Long, Ayoze Perez, Mohamed Salah na Chris Wood.