Mnyama kutua Dar leo akitokea Mbeya
Kikosi cha Simba SC kinarejea jijini Dar es Salaam mchana wa leo baada ya kuwa na michezo miwili ya Ligi kuu Tanzania bara Jijini Mbeya.
Simba SC alikutana na Mbeya City Mei 3 na kushinda goli 2-1 na Mei 5 alikutana na Tanzania Prisons na kuondoka na ushindi wa goli 1-0 na hivyo kujichukulia pointi 6 jijini Mbeya.
Simba SC sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu kwa kuwa na pointi 78 huku wakiwa wamepishana pointi mbili na Dar es Salaam Yanga Afrika mwenye point 80.