Bado pointi 4 tu Samatta kubeba ubingwa Ubelgiji
Inawezekana kabisa msimu wa 2018/2019 ukawa wa kihistoria kwa mtanzania Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika timu ya KRC Genk , Samatta anaweza kuandika historia kwa kutwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu ya Ubelgiji toka atue katika ardhi hiyo.
.
Matumaini ya KRC kutwaa taji hilo yanawezekana kutokana na uhitaji wao wa alama nne tu zinawafanya wawe Mabingwa wakati huu wakiwa wametoka kuzikusanya alama tatu dhidi ya Antwerp FC waliomfunga mabao 4-0, Mbwana Samatta akifunga la pili dakika ya 55 katika ushindi huo.
.
Mbwana Samatta anaongoza na kukaribia kutwaa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora kwa kufunga magoli 23 hadi sasa akifuatiwa na Mtunisia Hamdi Harbaoui wa Klabu ya Zulte Walegen kwa kufunga magoli 18, Samatta amempita magoli 5 hivyo ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora.
.
Kwa upande wa Kombe la Ligi Kuu nchini Ubelgiji wanalowania kwa kuwa wamefikisha alama 50 katika michezo ya Play Offs, sasa wanahitaji alama 4 tu ili wafikishe alama 54 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, hivyo kama watapata matokeo chanya katika mechi zao tatu zijazo wakishinda mbili au ushindi moja na sare moja watakuwa wametangazwa Mabingwa wakiwa na mchezo mmoja mkononi.