Cristiano Ronaldo autaka ukocha
Nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo baada ya kufanikiwa kuisaidia timu yake ya Juventus kushinda taji lake la nane mfululizo la Serie A, ameeleza kuwa anapenda kuishi Italia na kuna uwezekano pia wa kuendelea kuishi huko baada ya kustaafu na kuanza kazi ya ukocha.
.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa na mwanzo mzuri kiasi akiwa na Juventus akiwa amefunga jumla ya mabao 26 katika mashindano yote msimu huu akiwa na timu hiyo na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuwahi kushinda taji la EPL, LaLiga na Serie A katika historia ila ameshindwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.
.
“Kitu cha kwanza ninachofanya pale ninapopata timu mpya ni kuwa mwenyewe na sio kingine chochote, kama upo ‘smart’ kuna vitu unapata vinavyoweza kukuimarisha kama mwanamichezo “ aliongea kupitia jarida la ICON la Hispania.
Alipoulizwa kuhusiana na uwezekano wa kuwa kocha akistaafu Ronaldo alijibu “Siwezi kulikataa hilo” akimaanisha inawezekana kuifanya kazi hiyo.
.
Ni wachezaji wachache sana ambao wamewahi kucheza soka kwa kiwango cha juu, baada ya kustaafu kwao soka wamefanya kazi za ukocha wengi wao wamekuwa wakiendelea na maisha mengine kama Ronaldo De Lima, Ronaldinho, Pele, Jay Jay Okocha wakati kama Maradona aliyeamua kufanya kazi ya ukocha amekuwa akichemka mara kadhaa licha ya umahiri wake enzi anacheza soka.