D’Angelo Russell akamatwa na bangi uwanja wa ndege
Staa wa timu ya Brooklyn Nets ya NBA ,D’Angelo Russell amekamatwa na gram 50 za marijuana katika uwanja wa ndege wa LaGuardia huko New York.
Maafisa wa uwanja wa ndege wakati wa ukaguzi walikuta mzigo huo wa Marijuana ambao alikuwa ameuficha katika kopo la kuwekea chai.
Baadae mchezaji huyo aliachiwa na kupaa kuelekea Louisville, Kentucky sehemu aliyokulia na ndipo baba yake anapoishi.
Russell,23, aliandikiwa shauri na anahitajika kufika mahakamani.
.
‘ Tunafahamu kilichotokea kuhusiana na D’Angelo Russell na tunafanya mchakato kukusanya taarifa zaidi kwa wakati huu’ timu ya Nets imetoa taarifa hiyo.