Wenger ashusha lawama zake kwa Van Dijk
Kocha wa zamani wa timu ya Arsenal ya nchini England aliyedumu na timu hiyo kwa miaka 22 Arsene Wenger, ameamua kuelekeza lawama zake za mchezo wa Barcelona dhidi ya Liverpool wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa beki wa Liverpool Virgil Van Dijk.
Wenger amekosoa na kueleza kuwa goli lililokuwa limewaweka Liverpool katika nafasi mbaya na kucheza kwa presha ni goli la kwanza la FC Barcelona lililofungwa na Luis Suarez dakika ya 25 ya mchezo katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Liverpool.
.
“Barcelona wanapofika sehemu ya tatu ya mwisho wana ubora sana, Van Dijk alikaba lakini alitakiwa angeenda pamoja na Suarez kuokoa ule mpira, hususani beki wa kati wa kiwango kama chake, anamuacha (Suarez) , kutokea mwanzo katika nafasi yake sio mbaya lakini alikataa kwenda kukaba” Wenger akiongea na beinSPORTS baada ya Van Dijk kukabia macho goli la Suarez