Klopp ampa heshima Lionel Messi mbele ya Pele
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameeleza dhamira yake ya kumaliza ndoto za Lionel Messi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa May 1 huku akiwaambia wachezaji wake kuwa lazima wawe na tahadhari na wakubali kuhangaika.
Klopp kasema hivyo akiwa na maana ya kutaka kuwaondoa Barcelona na kuzima ndoto ya nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi ambaye aliahidi Septemba 2018 kuwa watatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, pamoja na hayo Jurgen Klopp hajaondoa heshima kwa mchezaji huyo na kusema ndio bora kwake.
.
“Messi kwangu mimi ndio namuona mchezaji namba 1 kwa asilimia 100 hiyo ni kwa mtazamo wangu, tunalazimika pia kusema Cristiano Ronaldo yupo lakini na wengine pia tunapaswa kuwatazama.”
.
“ Siku zote baba yangu alikuwa akiniambia ni Pele ndio mchezaji bora lakini sikuwahi kumuona Pele ‘live’ akicheza ,nilikuwa mdogo kipindi hicho, kwa upande wangu mimi Lionel Messi ndio bora” alisema Jurgen Klopp kuelekea mchezo huo wa nusu fainali