Kinda wa Tanzania asajiliwa Arsenal
Nyota kinda ambaye ni zao pia la timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys iliyoshiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana nchini Gabon 2017, Yohana Mkomola amefanikiwa kusaini dili huko barani Ulaya.
Yohana Mkomola ambaye amewahi kuichezea Yanga pia baaadae African Lyon amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kucheza soka la kulipwa nchini Ukraine katika klabu ya Arsenal Kiev ya nchini Ukraine.
Mkomola ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji kwa sasa ana umri wa miaka 18 akielekea 19, amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kufuzu majaribio katika klabu ya Arsenal Kiev inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ukraine ila kwa sasa ipo katika hali mbaya na inawezekana ikashuka daraja baada ya kucheza msimu mmoja Ligi Kuu ma kurudi Ligi daraja la kwanza.